16 Februari 2026 - 14:10
Vijana 250 Washiriki Semina ya Wajibu Katika Kipindi cha Ghaibah Kubwa +Dodoma

Semina hiyo iliyoandaliwa na wanafunzi wa Kishia wa vyuo vikuu mjini Dodoma kwa ushirikiano na Bilal Muslim Mission of Tanzania ilijikita katika kuwakumbusha vijana wajibu wao wa kiimani, kimaadili na kijamii katika kipindi cha Ghaibah ya Imam Mahdi (a.t.f.s), huku takribani vijana 250 wakishiriki.

Vijana 250 Washiriki Semina ya Wajibu Katika Kipindi cha Ghaibah Kubwa +Dodoma

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Alhamdulillah, nimebarikiwa kushiriki na kuwasilisha mada katika semina ya vijana iliyoandaliwa na wanafunzi wa Kishia wa vyuo vikuu mjini Dodoma kwa ushirikiano na Bilal Muslim Mission of Tanzania.

Mada ya semina hiyo ilikuwa: “Wajibu wa Vijana katika Kipindi cha Ghaibah ya Imam Mahdi (a.t.f.s)”, ambapo takribani vijana 250 walishiriki.

Your Comment

You are replying to: .
captcha